Machapisho Maarufu

Jumapili, 14 Aprili 2013

SAFARI YA DALAJA LA MUNGU(GOD'S BRIDGE TOUR)

 Wanachama wa chama cha mabalozi mbeya town walitembelea  dalaja la mungu lililopo tukuyu wilaya ya rungwe mkoa wa mbeya.
 dalaja hilo lina aminika kuwa ni la asili yaani lilijengwa na mungu.halikadhlika kisayansi inaaminika kuwa daraja hilo lilitokana na msukumo mkubwa wa maji ambayo yalipelekea kutoboka kwa mwamba.haya ni maoni kutoka kwa baadhi ya wanachama.
 issa yahaya alisema"mimi kwanilivyoona dalaja hili limetokana na volcano ilitoka kwenye mlima rungwe ambayo ilishuka na kupita kwenye mto kiwila" yeya anaamini kuwa volcano ilitoboa mwamba na kutengeneza daraja lile.
 mwanachama mwingine anayefahamika kama HOSEA MWASIPOSYA alisema" vitu vya asili kama hivi hatupaswi kuumiza akili sana bali tunatakiwa kumuachia MUNGU na siku tutakayokuwa mbinguni atatupatia majibu"
wakiwa eneo la daraja la mungu, wanachama walijifunza mambo mbalimbali kama masomo ya unabii,ukuaji na kubalehe pamoja na mavazi na mitindo ya maisha.
baada ya kutoka daraja la mungu mabalozi walipata nafasi ya kutembelea sehemu nyingine ya kitalii iitwayo "KIJUNGU" sehemu hii ilionekana kushangaza watu kutoka na mfumo mzima wa maji wa asili ulioonekana pale
..baada ya hapo ulikuwa ni wakati wa kumshukuru mungu kwa safari ile..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni